Fisi Madoa Apata Ukoo Mpya

Kujali, ni fisi madoa aliyehama ukoo wake kwenda kutafuta ukoo mwingine mpya.

Safari yake ni ya ujasiri, ukakamavu,na kutokata tamaa, ikituonyesha sifa za ajabu za hawa wanyama wa kipekee na wakuvutia.

Hadidhi hii imetungwa kwa ushauri na ushirikiano wa Dr. Eve Davidian na Dr. Oliver Höner kutoka Mradi wa Fisi, Hyena Project, ambao kwa pamoja ni sehemu ya timu ya kimataifa ya biolojia tabia waliofanya utafiti wa fisi madoa nchini Tanzania kwa takribani tangu 1996.

Hizi n baadhi ya tabia za kipekee za fisi ambazo hadidhi hii imezingatia:
  • Kama ilivyo kwa Kujali, fisi dume mara nyingi huondoka na kuacha ukoo waliozaliwa na huwa inachukua muda na majaribio kadhaa kabla ya fisi hao kukubaliwa na ukoo mpya.

  • Fisi wanawasiliana kwa kutumia sauti mbali mbali. Mlio wa “wuupsi”  unatumika kwa mawasiliano ya mbali. Wanatumia mlio unaofanana na “kicheko” au ‘kuchekacheka” wanapokua na hofu au mkazo wa mawazo.

  • Kwenye jamii za fisi ukoo unatokana na upande wa mama na mpangilio wa uongozi na vyeo ni wa utawala wa msonge; waliokua kwenye sehemu ya juu ni wanawake.

Tafsiri kwa lugha ya Kiswahili: M.K. Nicholas Mchawala

  • Fisi wanakula mabaki na kusaidia kupunguza magonjwa, tabia hii inawapa jina la “Wasafishaji wa mbuga.”

  • Ukoo wa fisi unapangwa kwenye msingi wa kusaidiana kazi kama timu. Wanasaidiana na kujenga mahusiano yenye nguvu, ya kirafiki, na pia kuwa na ushirikiano ni muhimu kwao.

  • Majina ya Jasiri na Malkia ni ya Kiswahili, lugha ya taifa ya Tanzania, nchi yenye idadi kubwa ya fisi madoa kuliko nchi nyingine zote duniani